Mkuu wa wauguzi hapa jijini Nairobi amepuuzilia mbali taarifa kwamba wauguzi wangeungana na madaktari katika kuishinikiza serikali kutimiza matakwa yao. Boaz Onchari amesema hakuna sheria inayosema waungane na madaktari wanapogoma huku akishtumu wanaompiga vita katibu mkuu wa wauguzi Seth Panyako.