Naibu msemaji wa serikali Mwanaisha Chidzuga amesema serikali ya Rais William Ruto imejitolea kuhakikisha wakenya wanalindwa kutokana na majanga hasa mafuriko.
Akiongea na Radio Taifa, Chidzunga amesema serikali imeweka mikakati mbali mbali kando na kuwahamisha wakenya na kuwapa makao wakenya walioathirika na mafuriko, serikali pia inatoa fedha kwa waathiriwa. Aidha amewasihi wakenya na mashirika mbali mbali kuungana ili kusaidia wakenya zaidi.