Mchambuzi wa masuala ya siasa Martin Andati anasema kuwa pendekezo la seneta mteule Chimera Mwinzagu la kuwazuia magavana waliohudumu katika wadhifa huo kutogombea tena viti vya kisiasa halitafua dafu.
Kulingana na Andati, pendekezo hilo litakuwa linakiuka haki zao za kikatiba.