Home Vipindi Zinga: Demokrasia ya Vyama na Pendekezo la kuongeza muhula wa Rais ,...

Zinga: Demokrasia ya Vyama na Pendekezo la kuongeza muhula wa Rais , mwelekeo ni upi ?

0

Wakati ambapo mazungumzo ya maridhiano yanaendelea, Upinzani umeonekana kukemea Serikali dhidi ya kunyakua wabunge wao kwa kuwaalika katika Ikulu jambo ambalo Upinzani unasema unatishia demokrasia ya vyama na taifa kwa jumla.

Kulingana na Mbunge wa Bomachoge Borabu Nofalson Barongo mchakato wa Kenya Kwanza unatishia hatua za demokrasia, hata hivyo anasema mazungumzo ya maridhiano yanafaa kupewa heshima yake kwani yameunganisha taifa jambo ambalo mchambuzi wa masuala ya Siasa David Alulu amepinga na kusema mazungumzo hayo huenda yakakosa kuafiki lengo la Upinzani.