Home Habari Kuu Ziara ya Mfalme Charles kuimarisha biashara nchini

Ziara ya Mfalme Charles kuimarisha biashara nchini

Rais alimwambia Mfalme kwamba yeye si mgeni nchini Kenya, kwani amewahi kutembelea mwaka wa 1971, 1977, 1978 na 1987.

0
Mfalme Charles wa tatu wa Uingereza.

Kenya itaongeza uhusiano wake na Uingereza ili kuimarisha biashara na uwekezaji.

Rais William Ruto amesema nchi hizo mbili zina uhusiano tajiri, thabiti na wa kihistoria, ambao lazima utumiwe kwa maslahi yao ya pamoja.

Alibainisha kuwa Kenya na Uingereza zina nia ya kufanya kazi pamoja ili kupanua ushirikiano wao katika maeneo ya kimkakati.

Mambo hayo, alibainisha kuwa ni pamoja na ulinzi na usalama, elimu, uhifadhi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

Alisema hayo siku ya Jumanne wakati wa mazungumzo ya faragha na Mfalme Charles III katika Ikulu ya Nairobi.

Hapo awali, akiwa na Mke wa Rais Rachel Ruto, Mkuu wa Baraza la Mawaziri Musalia Mudavadi, na viongozi wengine, Rais aliwakaribisha Mfalme na Malkia walipoanza ziara yao nchini Kenya.

Rais alimwambia Mfalme kwamba yeye si mgeni nchini Kenya, kwani amewahi kutembelea mwaka wa 1971, 1977, 1978 na 1987.

Walakini, hii ni ziara ya kwanza ya Mfalme katika taifa hili la Jumuiya ya Madola kama Mfalme.

Ni Kenya ambapo utawala wa Malkia Elizabeth II ulianza, baada ya kutwaa kiti cha enzi mnamo Februari 1952.

“Tunashukuru juhudi ulizofanya kuanzisha, kudumisha na kukuza uhusiano wako nasi,” alieleza Rais.

Familia hiyo ya kifalme, katika taarifa, ilibaini kuwa ziara hiyo ni ya kumbukumbu nzuri na inalenga kusherehekea uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili.

Katika bustani ya Uhuru, Mfalme alitoa heshima zake kwa mashujaa wa Kenya walioaga dunia kwa kuweka shada la maua kwenye kaburi.