Home Habari Kuu Zana za vita za Marekani zawasili Israel

Zana za vita za Marekani zawasili Israel

Kundi la washambuliaji la USS Gerald R Ford pia limewasili Mashariki mwa Mediterania.

0
kra

Ndege ya kwanza iliyobeba zana za kijeshi za Marekani imewasili katika Kambi ya Nevatim kusini mwa Israel, kulingana na mamlaka za eneo hilo.

“Ushirikiano kati ya wanajeshi wetu ni sehemu muhimu ya kuhakikisha usalama wa kikanda na utulivu wakati wa vita,” Jeshi la Ulinzi la Israeli lilisema katika taarifa iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.

kra

Kundi la washambuliaji la USS Gerald R Ford pia limewasili Mashariki mwa Mediterania.

Hayo yanajiri huku Marekani ikizungumza na Israel na Misri kuhusu njia salama kwa raia wa Gaza huku Israel ikiendelea kuishambulia Palestina.

“Tumezingatia swala hili, kuna mashauriano yanaendelea,” mshauri wa usalama wa kitaifa wa Marekani Jake Sullivan aliwaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani.

Sullivan hakutoa maelezo zaidi, akisema tu kwamba majadiliano “kati ya mashirika ya uendeshaji” yanaendelea.

Wizara ya Afya ya Gaza imesema Wapalestina wasiopungua 900 wameuawa na hadi 4,600 wamejeruhiwa tangu Jumamosi juma lililopita.