Home Kimataifa Zaidi ya wauguzi 500 wa Kenya kuhudumu Saudi Arabia

Zaidi ya wauguzi 500 wa Kenya kuhudumu Saudi Arabia

0

Zaidi ya wauguzi  580 wakenya waliohitimu wametayarishwa kuondoka nchini kuhudumu nchini Saudi Arabia.

Wiziri wa leba Florence Bore alisema watahiniwa ambao waliafikia mahitaji yote wanatarajiwa kufanyia duru ya mwisho ya mahojiano tayari kuondoka nchini.

Aidha alisema baraza la wauguzi nchini limewaidhinisha wauguzi hao kwenda kuhudumu nje ya nchi.

Mnamo mwezi Januari, wizara ya leba ilitoa wito kwa wauguzi waliohitimu kutuma maombi kwa nafasi za kazi 2,500 nchini Saudia kwenye mkataba baina ya mataifa hayo mawili utakaohakikisha wafanyakazi wa Kenya wanahudumu nchini humu kwa mazingira salama.

Waliotarajiwa kutuma maombi ya kazi ni wauguzi wa kawaida, wasaidizi wa kibinafsi na wasaidizi wa huduma za afya.

Bore aliyefika mbele ya kamati ya bunge kuhusu maswala ya kigeni na uhamisho wa wafanyakazi, inayoongoza na Lydia Haika, alisema ni maombi 1,765 yaliyopokelewa yakijumuisha wanawake 880 na wanaume 885.

Website | + posts