Home Habari Kuu Zaidi ya watu 50 waripotiwa kufariki kwenye bwawa la Mai Mahiu

Zaidi ya watu 50 waripotiwa kufariki kwenye bwawa la Mai Mahiu

0

Zaidi ya watu 50 wameripotiwa kuaga dunia kutokana na mkasa wa kupasuka kwa bwawa la Mai Mahiu mapema Jumatatu.

Bwawa la Old Kijabe lilivunja kingo zake mapema Jumatatu na kusomba magari,nyumba,watu na mifugo, huku jumla ya miili 45 ikiwemo ya watoto 17 ikipatikana kwenye eneo la mkasa.

Bwawa hilo la umbali wa kilomita 20 lilivunja kingo zake na kumwaga maji kwa vijiji vilivyo karibu.

Mamia ya wakazi wameachwa bila makao baada ya nyumba zao kubebwa na maji ya mafuriko ya bwawa hilo.

Kulingana na msemaji wa serikali Isaack Mwaura watu 66 wameripotiwa kuaga dunia kote nchini kutokana na visa mbalimbali vya mafuriko.

Website | + posts