Home Michezo Timu zaidi ya 300 kushiriki makala ya kwanza ya Sakaja Super Cup

Timu zaidi ya 300 kushiriki makala ya kwanza ya Sakaja Super Cup

Timu mshindi kwa wanaume itatuzwa shilingi milioni 3, nambari mbili shilingi milioni 2 na milioni moja kwa timu ya tatu.

0

Timu zaidi ya 300 za kaunti ya Nairobi zitashindana katika kipindi cha miezi miwili unusu katika makala ya kwanza ya mashindano ya Sakaja Super Cup.

Mashindano hayo yalizinduliwa jana Jumatano jioni katika ukumbi wa Charter na Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnstone Sakaja.

Sakaja aliwarai vijana kutumia vyema fursa hiyo kuboresha maisha yao.

Jumla ya timu 340 zimejiandikisha kushiriki kutoka maeneo yote ya kaunti ya Nairobi huku fainali yake ikipangiwa kuchezwa Disemba 16.

Timu mshindi kwa wanaume itatuzwa shilingi milioni 3, nambari mbili shilingi milioni 2 na milioni moja kwa timu ya tatu.

Kwa upande wa akina dada, mabingwa watatunukiwa shilingi milioni 1, nafasi ya pili nusu milioni na elfu 250 kwa timu ya tatu.