Home Kaunti Zaidi ya miti 5,000 yapandwa kaunti ya Busia

Zaidi ya miti 5,000 yapandwa kaunti ya Busia

Miche hiyo ilijumuisha ile ya kiasili pamoja na mianzi.

0
Zaidi ya miti 5,000 yapandwa kaunti ya Busia.

Zaidi ya miti 5,000 imepandwa katika kaunti ya Busia wakati wa zoezi la kitaifa la upanzi wa miti siku ya Ijumaa.

Afisa mkuu wa uhifadhi wa misitu wa kaunti hiyo   Vitalis Osodo, alisema miche hiyo ilijumuisha ile ya kiasili pamoja na mianzi.

“Ninafuraha kusema kuwa tumepanda miti 5,000 ya kiasili na 250 ya mianzi yote ikiwa miti 5,250,” alisema Osodo.

Aidha afisa huyo wa misitu alisema kaunti hiyo inahitaji kushirikiana na wadau wengine kuafikia asilimia 30 ya utandu wa misitu kufikia mwaka 2031.

“Lengo la kaunti ya Busia ni kupanda miti kwa ardhi ya ekari 50,000 kufikia mwaka 2032, hii ikiwa ni asilimia 27,” alisema Osodo akiashiria kuwa kiwango cha miti katika kaunti hiyo ni cha asilimia 8.3.

Kamishna wa eneo la Magharibi Irungu Macharia, aliwashauri wakazi wa eneo hilo kupanda miti katika maeneo ya miinuko, ili kuzuia mmomonyoko wa udongo.