Home Michezo Yego akosa kufuzu kwa fainali ya urushaji sagai

Yego akosa kufuzu kwa fainali ya urushaji sagai

0

Bingwa wa dunia mwaka 2015 katika urushaji sagai Julius Yego amekosa kufuzu wka fainali ya makala ya mwaka huu mjini Budapest, Hungary.

Yego alibanduliwa katika hatua ya mchujo baada ya kurusha sagai umbali mita 78 nukta 42 akimaliza wa nane.

Ili kujikatia tiketi kwa fainali ya urushaji sagai, mwanariadha alihitajika kurusha umbali wa mita 83 au kuwa miongoni mwa 12 bora.

Yego aliye na umri wa miaka 34 alifuzu kwa mashindano ya mwaka huu ya dunia kutokana na kuwa katika nafasi bora barani Afrika.

 

 

Website | + posts