Home Michezo Yanga yailemaza Simba kwa kuibinikiza 5-1 Kariakoo derby

Yanga yailemaza Simba kwa kuibinikiza 5-1 Kariakoo derby

0

Yanga wameigaragaza Simba mabao matano kwa moja katika derby ya Kariakoo, kuwania alama 3 za Ligi Kuu Tanzania bara iliyosakatwa Jumapili jioni katika uchanjaa wa Benjamin Mkapa.

Kennedy Musonda aliwaweka Yanga uongozini kunako dakika ya 3, kabla ya Denis Kibu kuwasawazishia Simba kunako dakika ya 9 na kipindi cha kwanza kumalizikia sare ya 1-1.

Kipindi cha pili hali ilikuwa ngumu kwa mnyama Simba akikaliwa kimabavu na Jangwani Boys, Mpia Nzengeli akitikisa nyavu mara 2 nao Stephane Aziz Ki na Peodoh Pacome Zouzoua wakaongeza moja kila mmoja na kuhitimisha kipigo cha kihistoria cha mabao 5-1.

Yanga wangali kushikilia kukutu uongozi wa ligi hiyo kwa alama 21 kutokana na mechi 8,pointi 3 zaidi ya watani Simba wanaokalia nafasi ya tatu.

Website | + posts