Waakilishi wa Afrika Mashariki katika hatua ya makundi ya kipute cha Ligi ya Mabingwa Young Africans kutoka Tanzania,watakabiliana na mabingwa mara tano TP Mazembe ya DRC kulingana na droo ya makundi iliyoandaliwa Jumatatu.
Young Africans ukipenda Yanga wamejumuishwa kundi A pamoja na Al Hilal SC ya Sudan na MC Alger kutoka Algeria.
Mabingwa wa mwaka 2016 Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini wamo kundi B pamoja na mabingwa mara tatu Raja Athletic Club na ASFAR Club zote za Morocco na limbukeni AS Maniema ya DR Congo.
Kundi C linasheheni Mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri ,CR Belouizdad ya Algeria, Orlando Pirates kutoka Afrika Kusini na Stade d’Abidjan ya Ivory Coast huku kundi D likiwa na Esperance ya Tunisia, Pyramids ya Misri na Sagrada Esperanca ya Angola.
Kundi A:TP Mazembe,Young Africans,Al Hilal SC,MC Alger
Kundi B:Mamelodi Sundowns,Raja Athletic Club,ASFAR Club,AS Maniema Union
Kundi C:Al Ahly SC,CR Belouizdad,Orlando Pirates,Stade d’Abidjan
Kundi D:Esperance,Pyramids,Sagrada Esperanca,Djoliba AC De Bamako
Katika kombe la Shirikisho miamba wa Tanzania Simba SC wamo kundi A pamoja na CS Constantine ya Algeria na CS Faxien kutoka Tunisia na Bravos do Marquis from Angola.
RS Berkane ya Morocco imo kundi B pamoja Stade Malien ya Mali, Stellenbosch kutoka Afrika Kusini na CD Lunda ya Angola.
USM Alger ya Algeria imo kundi C pamoja na Asec Mimosas kutoka Ivory Coast, Jaaraf ya Senegal na Orapa United ya Botswana.
Mabingwa watetezi Zamalek Misri , Enyimba kutoka Nigeria, Al Masry ya Misri na na Black Bulls kutoka Musumbiji .
Kundi A: Simba SC, CS Sfaxien, CS Constantine, FC Bravos do Maquis
Kundi B: RS Berkane, Stade Malie, Stellenbosch, CD Lundal Sul.
Kundi C: USM Alger, ASEC Mimosas, ASC Jaraaf, Orapa United
Kundi D: Zamalek SC, Al Maseh, Enyimba, Black Bulls.
Mechi hizo zitachezwa kaunzia wiki ya mwisho ya mwezi Oktoba na kukamilika Januari mwaka ujao.