Wydad Casablanca wakicheza nyumbani walisajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ,katika duru ya kwanza ya fainali ya kombe la Ligi ya Soka Afrik,AFL Jumapili usiku katika uchanjaa wa Mohammed V.
Rivaldo Coetzee alijifunga bao la dakika ya 41 na kuwapa wenyeji uongozi wa kipindi cha kwanza.
Abdelmounaim Boutoui alisawazishia wageni Masandawana katika dakika ya 73 kupitia penati kufuatia difenda Jabrane kuunawa mpira.
Dakika tano baadaye kiungo Anas Serrhat, alifyatua tobwe akiwa ndani ya kijisanduku na kuwapa Wydad bao la ushindi.
Duru ya pili itapigwa Jumapili ijayo mjini Pretoria huku mshindi wa jumla akituzwa shilingi milioni 600 na shilingi milioni 450 kw timu itakoyoshindwa.