Home Michezo Wydad kuwaalika Mamelodi katika duru ya kwanza ya fainali kombe la AFL...

Wydad kuwaalika Mamelodi katika duru ya kwanza ya fainali kombe la AFL Jumapili

0
Entertainment during the 2023 African Football League match match between Simba SC and Al Ahly SC in Benjamin Mkapa National Stadium in Dar es Salaam, Tanzania on 20 October 2023 ©BackpagePix

Wydad Casablanca ya Morocco itawaalika Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika mkondo wa kwanza wa fainali ya kombe la AFL Jumapili Novemba 5, kuanzia saa tatu usiku katika uwanja wa Mohammed V mjini Casablanca Morocco.

Mkondo wa pili utaandaliwa  nchini Afrika Kusini huku timu mshindi ikitunukiwa shilingi  milioni 600 za Kenya na milioni 450 kwa timu itakayomaliza nafasi ya pili.

Mashindano hayo ambayo ni ya makala ya kwanza yameshrikisha vlabu vinane bora barani Afrika, na yanafadhiliwa na Kinara wa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA Gianni Infantino.

Ili kutinga fainali Mamelodi iliwabandua washindi  mara 11 wa ligi ya mabingwa  Afrika ,Al Ahly ya Misri kwa ushindi wa bao 1 kwa nunge, nao Wydad Casablanca wakaitema nje Esperance ya Tunisia penati 5-4, kufuatia sare ya bao moja kutokana na mikumbo miwili.

Mikondo yote miwili ya fainali itarushwa mubashara kupitia runinga ya taifa KBC Channel 1.

Website | + posts