Home Kimataifa Wizara zatakiwa kupunguza bajeti zao kwa asilimia 10

Wizara zatakiwa kupunguza bajeti zao kwa asilimia 10

0
kra

Rais William Ruto ameziagiza wizara kupunguza bajeti zao za mwaka 2023/2024 kwa asilimia 10 ili kuhakikisha matumizi ya wizara hizo yanawiana na rasilimali zilizopo wakati kukiwa na mdororo wa uchumi duniani. 

Amesisitiza haja ya serikali kutumia rasilimali ipasavyo, akikariri kuwa matumizi mabaya na ufisadi havitakubaliwa kamwe.

kra

Akizugumza alipoongoza mkutano wa Baraza la Mawaziri katika Ikulu ya Nairobi, Rais Ruto alionya maafisa wa serikali wanaokusudia kukwepa matumizi ya mfumo mmoja wa kufanya malipo akisisitiza umuhimu wa uangalizi mzuri.

Na ili kuepusha kuyumba kwa bei, iliamuliwa kuwa serikali itatenga shilingi bilioni 4 kununua mahindi kutoka kwa wakulima.

Baraza la Mawaziri lilielezea umuhimu wa kuwasaidia wakulima kukausha na kuhifadhi mahindi ili kuepusha hasara zinazotokea baada ya uvunaji wa zao hilo.

Aidha, baraza hilo liliidhinisha Sera ya Uchezaji Kamari 2023, Mswada wa Udhibiti wa Uchezaji Kamari, 2023 na Mswada wa Kitaifa wa Bahati Nasibu, 2023 ambayo itawasilishwa bungeni.

Miswada hiyo inalenga kutumiwa kama mpangokazi wa kubadilisha sekta ya uchezaji kamari kuwa nguzo muhimu katika uendelezaji wa jamii.

Website | + posts