Home Habari Kuu Wizara ya Elimu: Hatujabadili tarehe ya likizo ya katikati ya muhula

Wizara ya Elimu: Hatujabadili tarehe ya likizo ya katikati ya muhula

0
Katibu wa Elimu ya Msingi Dkt. Belio Kipsang
Katibu wa Elimu ya Msingi Dkt. Belio Kipsang
kra

Wizara ya Elimu imepuuzilia mbali madai kuwa imebadilisha tarehe ya likizo ya katikati ya muhula wa pili kwa wanafuzi kote nchini. 

Wizara ilitoa taarifa hiyo baada ya mtandao mmoja wa habari kudai kuwa serikali imebadili tarehe ya kuanza kwa likizo hiyo. Mtandao huo ulidai likizo hiyo sasa ingeanza leo Jumatatu.

kra

Lakini Wizara inasema mabadiliko yaliyotangazwa Mei 24, 2024 yangalipo na hayajafanyiwa mabadiliko kivyovyote.

Katika mabadiliko yaliyotangazwa Mei 24, 2024, serikali ilitangaza kuwa wanafunzi sasa wataenda kwenye likizo ya katikati ya muhula wa pili kati ya Juni 26-28, 2024.

Awali, wanafunzi walipangiwa kwenda kwenye likizo hiyo Juni 20-2024 mwaka huu.

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, wanafunzi wa shule za mabweni watahitajika kuripoti shuleni Juni 30.

Ufunguzi wa shule kwa muhula wa pili ulicheleweshwa kwa takriban wiki moja  kutokana na mvua kubwa iliyosababisha mafuriko na kuathiri mijengo mingi ya shule.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here