Home Kimataifa Wizara ya Elimu kuchunguza mkasa wa moto katika shule ya Hillside

Wizara ya Elimu kuchunguza mkasa wa moto katika shule ya Hillside

0
Shule ya Hillside Endarasha.
kra

Wizara ya Elimu imesikitishwa na mkasa wa moto uliosababisha vifo vya wanafunzi 17 katika shule ya sekondari ya Hillside Endarasha, kaunti ya Nyeri Alhamisi usiku.

Moto huo kulingana na taarifa ya Wizara ya elimu ulisababisha wanafunzi 14 kujeruhiwa wakiwa wanapokea matibabu katika hospitali mbalimbali .

kra

Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 824 wakiwemo wavulana 402 na wasichana 422 ambapo wavulana 156 na wasichana 160, wanaishi kwenye mabweni .

Bweni la wavulana ndilo lliliteketea na kusabisha vifo na majeraha kwa wanafunzi.

Wizara ya elimu inashirikiana na zile za usalama wa kitaifa na Afya , kuchunguza chanzo chazo moto huo na kudhibiti hali.

Rais William Ruto ambaye yuko ziarani nchini China ametuma risala za rambirambi kwa familia zilizoathiriwa, na kuamrisha kufanywa kwa uchunguzi wa haraka na wakina kuhusu mkasa huo wa moto.

Pia kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga ambaye yuko kwenye msafara wa Rais Ruto nchini China, ametoa rambirambi zake kwa familia zilizoathirika .

Website | + posts