Wizara ya Uwekezaji, Biashata na Viwanda itatekeleza jukumu muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi hii.
Waziri Rebecca Miano anasema wizara hiyo inalenga kuchangia asilimia 15 ya Pato Ghafi la Taifa, GDP kufikia mwaka 2027, mchango huo hasa ukitoka kwa sekta ya utengenezaji bidhaa.
“Dhamira hii inasimama kama kichocheo cha kweli cha ukuaji uchumi na kinaendana vyema na maono yetu ya Ajenda ya Mabadiliko ya Kiuchumi kuanzia Chini hadi Juu almaarufu BETA,” alisema Waziri Miano leo Jumatatu asubuhi.
Aliyasema hayo alipokutana na timu mbalimbali kutoka taasisi za idara ya viwanda iliyo chini ya wizara anayoongoza.