Waziri wa afya Susan Nakhumicha amesema serikali imetoa shilingi bilioni 6.1 kutimiza matakwa ya madaktari wanaogoma, huku akitishia kuwashtaki maafisa wa vyama vyao ikiwa hawatasitisha mgomo.
Maafisa wa vyama vya madaktari walikosa kujitokeza kwa mkutano ulioitishwa na serikali Jumanne kujadili maswala muhimu.
Waziri Nakhumicha ameapa kuwashtaki madaktari endapo hawatafutilia mbali mgomo ambao umeingia siku ya 41 Jumanne .
Kulingana na mkuu wa utumishi wa umma Felix Kosgei aliyeongoza kikao cha Jumatatu ,maswala 18 kati 19 ya madaktari yalisuluhishwa katika mkutano huo.
Serikali na madaktari walitarajiwa kusaini stakabadhi za kurejea kazini hali ambayo haikutimia kufuatia hatua ya madaktari kususia kikako hicho.
Ofa ya shilingi bilioni 6.1 waliyopewa madaktari ni ya pili baada ya ukataa ofa ya kwanza ya shilingi bilioni 2.4 ambapo madaktari wanagenzi walistahili kulipwa shilingi 70,000.
Hata hivyo chama cha madaktari nchini KMPDU kinataka wanagenzi hao walipwe shilingi 206,000 kwa mwezi