Home Kimataifa Wizara ya Afya yatetea kiwango cha matozo ya bima mpya

Wizara ya Afya yatetea kiwango cha matozo ya bima mpya

0

Wizara ya Afya imetetea kiwango cha asilimia 2.75 cha matozo ya wafanyakazi kwa ajili ya bima mpya ya afya almaarufu Social Health Insurance Fund – SHIF.

Waziri wa Afya Susan Nakhumicha anasema bima hiyo itafikia watu wengi zaidi lakini akaongeza kwamba wakenya wana haki ya kutoa maoni kuihusu kwenye vikao vya kushirikisha umma.

Anasema wana fursa ya kupendekeza kupunguzwa kwa matozo hayo huku akipuuzilia mbali dhana kwamba kiwango cha asilimia 2.75 ni hatua ya matajiri kulipia maskini.

Vikao vya kushirikisha umma kwenye suala la matozo ya bima mpya ya afya vinaendelea katika sehemu mbali mbali nchini ambapo Jumatatu Januari 29, 2024 Waziri nakhumicha ataongoza shughuli hiyo katika uwanja wa Mwatunge kaunti ya Taita Taveta.

Katika bima inayoondolewa ya NHIF walioajiriwa na ambao wana kiwango cha chini cha mshahara wamekuwa wakilipa kiwango kikubwa huku wenye mishahara mikubwa akilipa shilingi 1700 kila mwezi.

Chini ya SHIF kila aliyeajiriwa atatozwa asilimia 2.75 ya mshahara huku wale ambao hawajaajiriwa wakitoa kiwango sawia cha mapato yao mara moja kwa mwaka.

Website | + posts