Home Habari Kuu Wizara ya Afya yatangaza kuzuka kwa ugonjwa wa macho Mombasa

Wizara ya Afya yatangaza kuzuka kwa ugonjwa wa macho Mombasa

0
Katibu wa Afya ya Umma Mary Muthoni
Katibu wa Afya ya Umma Mary Muthoni

Wizara ya Afya imetangaza kuzuka kwa ugonjwa wa mboni ya macho katika kaunti ya Mombasa.

Kwenye taarifa, katibu wa afya ya umma katika wizara hiyo Mary Muthoni alisema  visa vingi vya matatizo ya mboni ya macho kugeuka kuwa mekundu vimeripotiwa katika kaunti hiyo.

Muthoni amesema ugonjwa huo huambukiza haraka sana na unasababisha macho kuwa mekundu, kuvimba, kuwasha na kuhisi kujikuna huku yakitoa uchafu.

Hata hivyo, kulingana na taarifa hiyo, chanzo cha ugonjwa huo hakijabainika huku uchunguzi ukiendelea maabarani.

Ugonjwa wa mboni ya macho husababishwa na bakteria, virusi na pengine kemikali, kwa mujibu wa taarifa hiyo.

Matatizo ya mboni ya macho husababishwa na uchafu, kutumia miwani chafu, maeneo yenye misongamano, familia zilizo na matatizo ya macho na hali mbaya ya hewa hususan msimu wa baridi .

Wizara ya Afya imeshauri umma kunawa mikono kwa maji na sabuni, kutumia sanitiza na kuzingatia usafi wa hali ya juu.

Waathiriwa pia wametakiwa kutembelea vituo vya afya na kujitenga nyumbani hadi dalila zitokee.

Website | + posts