Home Habari Kuu Wizara ya Afya yapokea chanjo za watoto

Wizara ya Afya yapokea chanjo za watoto

0

Wizara ya Afya imetangaza kuwasili kwa chanjo za watoto, baada ya taifa hili kukumbwa na upungufu wa chanjo hizo katika vituo vya afya.

Kupitia kwa taarifa, Katibu katika Idara ya Huduma za Matibabu Harry Kimtai alithibitisha kuwa wizara hiyo imepokea chanjo kadhaa zikiwemo zile za Polio,  Measles-Rubella, Tetanus-Diphtheria na BCG.

“Tunafuraha kutangaza kupokea chanjo 1,209,500 za Measles-Rubella, 3,032,000 za Poli (bOPV), 1,000,000 za Tetanus-Diphtheria na 3,129,000 za BCG,” alisema Kimtai.

Aliongeza kuwa chanjo hizo zinatayarishwa ili zisambazwe katika vituo tisa vya chanjo kote nchini.

Katibu huyo alitoa wito kwa wahudumu wa afya kushirikiana na makundi ya afya ya jamii kuhakikisha watoto ambao hawakuchanjwa, wanapelekwa katika vituo vya afya ili kuchanjwa.

“Tunawahimiza walezi kuwapeleka watoto kuchanjwa kwa kuwa chanjo hizo sasa zinapatikana.”

Website | + posts