Home Kimataifa Wizara ya Afya yapiga hatua katika kukabiliana na malaria

Wizara ya Afya yapiga hatua katika kukabiliana na malaria

Asilimia 95 ya wakazi wa Homabay tayari wamepokea vyandarua vya kuzuia mbu. 

0
kra

Wizara ya Afya imeripoti kupiga hatua kubwa za ufanisi katika kampeni zake dhidi ya ugonjwa wa malaria. 

Kampeni hiyo ilizinduliwa mnamo Novemba 15 katika kaunti ya Homa Bay kwa lengo la kuwasilisha chanjo kwa wananchi wote na kupunguza visa vya ugonjwa wa malaria katika kaunti 22 zilizolengwa.

kra

Katika taarifa, katibu katika Wizara ya Afya Mary Muthoni alisema asilimia 95 ya wakazi wa Homa Bay tayari wamepokea vyandarua vya kuzuia mbu.

“Asilimia 95 ya waliolengwa kaunti ya Homa Bay wamepokea vyandarua,” alisema katibu Muthoni.

Katika kaunti ya Kisii, jumla ya vyandarua 841, 000 vimepokelewa, hali hii ikionesha uwajibikaji katika kuhakikisha vifaa mahususi dhidi ya ugonjwa huu vimetolewa.

Muthoni alisema pia wamezipa kipaumbele mbinu mwafaka kuhakikisha usafirishaji na uhifadhi salama chini ya halmashauri ya usambazaji vifaa vya kimatibabu nchini (KEMSA).

Mnamo mwezi Novemba, Wizara ya Afya ilizindua usambazaji mkubwa wa vyandarua vya kukabiliana na malaria vyenye dawa katika juhudi za kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huu.

Ripoti ya hivi karibuni humu nchini inaonesha takriban wakenya milioni 4 huugua malaria huku wengine zaidi ya elfu 10 wakiaga dunia kutokana na ugonjwa huo kila mwaka.

Website | + posts