Home Habari Kuu Wizara ya afya yachukua tahadhari dhidi ya mvua ya El Nino

Wizara ya afya yachukua tahadhari dhidi ya mvua ya El Nino

Kulingana na Muthoni kituo cha afya cha kushughulikia dharura kwa sasa kinatoa hamasisho kuhusu dalili za mapema na tahadhari za mvua ya El Nino.

0

Huku taifa hili likitarajia mvua ya El Nino, wizara ya afya imechukua hatua za tahadhari kwa kutambua maeneo ambako utoaji wa huduma za afya huenda ukakumbwa na chnagamoto.

Katibu katika idara ya afya ya umma Mary Muthoni, amesema wizara ya afya imeweka mikakati ya kushughulikia athari za mvua ya El Nino, ikiwa ni pamoja na kuimarisha uwezo wa vituo vya afya kukabiliana na magonjwa yanayosababishwa na maji, huku huduma za kawaida za afya zikiendelea kama kawaida.

Aidha kulingana na katibu huyo, serikali ya kitaifa inashirikiana na zile za kaunti zitaanzisha vituo vya muda vya matibabu katika maeneo ambapo watu watahitajika kuhamishwa pamoja na maeneo ambako vituo vya afya havitafikiwa kutokana na mafuriko.

Kulingana na Muthoni kituo cha afya cha kushughulikia dharura kwa sasa kinatoa hamasisho kuhusu dalili za mapema na tahadhari za mvua ya El Nino.

Muthoni alisema kampeni ya uhamasisho  kuhusu  magonjwa yanayoenezwa na maji kama vile homa ya Rift Valley, homa ya Dengue, Chikungunya pamoja na Malaria tayari unatekelezwa.