Home Habari Kuu Wizara ya Afya kuzindua utoaji chanjo dhidi ya HPV

Wizara ya Afya kuzindua utoaji chanjo dhidi ya HPV

Afisa mkuu mtendaji wa taasisi ya kitaifa kuhusu saratani ,Dkt. Elias Melly alitoa hakikisho kwa taifa kwamba chanjo hiyo ni salama.

Serikali kuzindua utoaji chanjo dhidi ya HPV.

Wizara ya Afya itazindua kampeni ya utoaji chanjo ya ugonjwa wa virusi vya Human Papilloma-HPV katika kaunti zote 47, katika juhudi za kukabiliana na ongezeko la visa vya saratani ya mlango wa uzazi humu nchini.

Afisa Mkuu tendaji wa taasisi ya kitaifa kuhusu saratani, Dkt. Elias Melly alitoa hakikisho kwa taifa kwamba chanjo hiyo ni salama.

Alidokeza kwamba takwimu za humu nchini zinaashiria kwamba kila mwaka, watu elfu 44 hugunduliwa na saratani ambapo 28,000 kati yao ni wanawake, ambapo wengi wao hugunduliwa na saratani ya mlango wa uzazi.

Dkt. Melly ambaye alikuwa akizungumza na wahudumu wa afya kwa jamii katika kaunti ya Bungoma, alisema kulingana na mahitaji ya Shirika la Afya Duniani – WHO, chanjo hiyo itatolewa kwa wasichana wenye umri wa miaka 15, huku wanawake wa umri kati ya 35 na 45 wakifanyiwa uchunguzi wa ugonjwa huo na wale watakaopatikana wameambukizwa watatibiwa.

Alitoa wito kwa wanawake kutilia maanani zoezi hilo la kupokea chanjo. Ugonjwa wa virusi vya HPV ni maradhi ya zinaa.

Website | + posts
Catherine Nyongesa
+ posts