Idadi ya watu waliofariki kutokana na vita kati ya Israel na wanamgambo wa Palestina katika eneo la Gaza imefikia watu 41, 534.
Hii ni kwa mujibu wa Wizara ya Afya katika eneo la Gaza linalodhibitiwa na kundi la Hamas.
Idadi ya waliofariki inajumuisha vifo 39 vilivyotokea saa 24 zilizopita.
Wizara hiyo imesema watu 96,092 wamejeruhiwa katika Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa mapigano yaliyotokana na shambulizi la kundi la Hamas nchini Israel Oktoba 7.
Vita kati ya Israel na wanamgambo wa Palestina kwa sasa vimeingia katika mwezi wake wa 12.