William Lai Ching-te ameapishwa kuwa Rais wa kisiwa cha Taiwan katika sherehe iliyokuwa na heshima zote kama kufyatuliwa kwa mizinga 21. Ching-te alisifia demokrasia ya kisiwa hicho kinachojitawala na akahimiza Uchina iache kukitishia.
Lai na makamu wake Hsia Bi-khim waliapishwa Jumatatu Mei 20, 2024 katika jumba la Rais na picha ya mwanzilishi wa taifa la China ROC Sun Yat-sen, ilikuwa imepachikwa katika eneo la uapisho.
Kiongozi huyo alipokezwa chapa mbili na spika wa bunge ambazo ni ishara muhimu za mamlaka ya Urais. Moja ni ya Republic of China – ROC jina rasmi la taifa hilo la Taiwan na nyingine ni ya heshima ya Rais.
Chapa hizo mbili zililetwa kisiwani humo kwa mara ya kwanza mwaka 1949 na wazalendo baada ya kushindwa kwenye vita na wakomunisti.
Rais anayeondoka Tsai Ing-wen alitumia fursa ya hafla hiyo kuaga rasmi baada ya kuwa mamlakani kwa mihula miwili ya jumla ya miaka minane.
Lai alikumbusha waliokusanyika kwa ajili ya uapisho wa leo umuhimu wa tarehe 20 mwezi Mei siku ambayo mwaka 1949, wakati sheria ya kijeshi ilianza kutekelezwa na tarehe sawia mwaka 1997 wakati Rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia aliapishwa kisiwani Taiwan.
Kiongozi huyo anayeondoka alisisitiza kwamba haitakubali mwingilio wowote kwa demokrasia yake na uhuru na akaitaka China kukoma kuingilia Taiwan na badala yake kuangazia amani na uthabiti.
China inadai kwamba Taiwan ni himaya yake na haijaashiria kwa vyovyote kwamba haitatumia nguvu kuafikia malengo yake kisiwani humo. Wakati wa uongozi wa Lai, China ilikuwa ikituma ndege pamoja na meli za kijeshi karibu na kisiwa hicho mtindo unaoendelea mpaka sasa.
Hafla ya uapisho wa Ching-te ilihudhuriwa na wawakilishi wa mataifa 29, wakiwemo mabalozi wa nchi 12 ambazo zilikuwa zimesalia kwenye uhusiano mwema na Taiwan katika maeneo ya Pacific, Amerika ya kati na Holy See.