Home Habari Kuu Wilfried Zaha ajiunga na klabu ya Galatasaray, Uturuki

Wilfried Zaha ajiunga na klabu ya Galatasaray, Uturuki

Galatasaray wanatarajiwa kurejea katika ulingo wa mashindano ya klabu bingwa barani ulaya msimu ujao ikiwa watashinda hatua ya tatu ya mchujo mwezi Agosti.

0

Winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha amejiunga na klabu ya Galatasaray nchini Uturuki kwa uhamisho huru baada ya mkataba wake na klabu ya Crystal Palace kufikia ukomo.

Galatasaray, mabingwa wa ligi ya Uturuki wanaelezwa kufikia makubaliano kukamilisha dili la Wilfried Zaha mwenye umri wa miaka 30 hapo jana kulingana na mtaalamu wa maswala ya soka na uhamisho, Fabrizio Romano.

Galatasaray ambao wanatarajiwa kurejea katika ulingo wa mashindano ya klabu bingwa barani ulaya msimu ujao ikiwa watashinda hatua ya tatu ya mchujo mwezi ujao wanasaka wachezaji wenye tajriba ikiwa ni pamoja na kuboresha kikosi chao kutetea ubingwa wao Uturuki.

Licha ya Klabu ya Crystal Palace kumwekea ofa mpya mezani ili aendelee kuitumikia, Zaha amependelea zaidi dili la Galatasaray ambao watashiriki michuano ya klabu bingwa barani ulaya msimu ujao.

 

 

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here