Home Habari Kuu Wetang’ula: Bunge halijatekwa nyara na serikali kuu

Wetang’ula: Bunge halijatekwa nyara na serikali kuu

Wetangula alisema bunge litaendelea kusimama imara katika utekelezaji wa jukumu lake la kutayarisha bajeti.

Spika wa bunge la taifa Moses Wetangula amewahakikishia wabunge kwamba bunge halitatumiwa kuidhinisha ajenda za serikali.

Akigusia maoni ya kiongozi wa wachache katika bunge hilo Opiyo Wandayi kuhusu uhuru wa kamati za bunge, Wetangula alisema bunge litaendelea kusimama imara katika utekelezaji wa jukumu lake la kutayarisha bajeti.

Spika huyo wakati huo huo, alitoa changamoto Kwa upande wa wachache bungeni, kutoa ushahidi kwamba serikali kuu imeiteka nyara bunge la kitaifa.

Wakati huo huo, serikali imependekeza marekebisho ya sheria ili kushirikisha halmashauri ya kukabiliana na uraibu wa pombe na mihadarati, NACADA kwenye maamuzi kuhusiana na utoaji leseni za uuzaji vileo.

Hatua hiyo inanuiwa kuhakikisha kanuni za kudhibiti uuzaji vileo zinazingatiwa kikamilifu katika juhudi za kuimarisha vita dhidi ya pombe haramu.

Mwenyekiti wa kamati ya usalama katika bunge la kitaifa Gabriel Tongoyo pia anatoa wito kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kusanifisha ushuru unaotozwa kemikali ya ethanol

Website | + posts
Radio Taifa
+ posts