Home Habari Kuu Wetang’ula asema bajeti ya shilingi bilioni 1.7 kufufua sekta ya sukari

Wetang’ula asema bajeti ya shilingi bilioni 1.7 kufufua sekta ya sukari

0

Spika wa Bunge la kitaifa Moses Wetang’ula amesema bajeti ya ziada ya shilingi bilioni 1.7 iliyopitishwa na wabunge itafufua sekta ya sukari nchini iliyokuwa imesambaratika.

Spika Wetang’ula amekanusha madai ya serikali kutaka kuuza kampuni ya kusaga miwa inayokabiliwa matatizo ya Nzoia Sugar, akisema shilingi milioni 300 ilizotengewa zitalipwa wakulima waliowasilisha miwa kiwandani.

“Viongozi wanaeza propaganda kuwa Nzoia sugar imeuzwa lakini ukweli ni kuwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo waziri wa kilimo Mithika Linturi atawasilisha shilingi milioni 300 kwa kampuni hiyo ili kugawiwa wakulima waliowasilisha miwa,aibu kwenu nyinyi mnaoeneza porojo.”Akasema Wetang’ula

Wetang’ula aliongeza kuwa shilingi milioni 250 zitalipa madeni ya wakulima huku milioni 50 zitakazosalia zikigharamia malimbikizi ya mishahara ya wafanyikazi.

Spika Wetang’ula alisema haya Ijumaa alipohudhuria mazishi ya Antony Namisi Maloba kijijini Mukhweya eneo bungela , Kabuchai.

Spika Wetang’ula aliandamana na wabunge seneta Wakoli Wafula,mwakilishi wa akina mama Catherine Wabiliang’a,John Chikati Martin Pepela,Ferdinand Wanyonyi,Majimbo Kalasinga na Kakai Bisau.

.

Website | + posts