Home Habari Kuu Wetangula ampongeza spika wa Zambia kwa uteuzi

Wetangula ampongeza spika wa Zambia kwa uteuzi

0
Spika Wetangula na Spika Mutti

Spika wa bunge la taifa nchini Kenya Moses Masika Wetangula, amempongeza mwenzake wa Zambia Nelly B.K. Mutti kwa uteuzi wake kwenye wadhifa huo akisema ni dhihirisho la uwezo alionao katika uongozi na maono.

Wetangula alimzuru spika huyo wa bunge la Zambia leo asubuhi, ambapo alitambua kwamba yeye ni mmoja wa maspika wachache wa kike ulimwenguni.

Anasema mazungumzo yao yaliangazia masuala ya ushirikiano, uwekezaji kati ya Kenya na Zambia na maendeleo ya utungaji sheria katika mabunge ya nchi hizo mbili.

Wawili hao walitambua uwezo mkubwa wa kiuchumi uliopo kati ya nchi hizi mbili na ushawishi wa mabunge yote mawili.

Spika Mutti awali alizuru bunge la Kenya na Wetangula anasema kwa pamoja watajibidiisha kukuza uhusiano wa kibunge ili kuendeleza ajenda ya kisheria ya Afrika.

“Mwingiliano huu unaashiria mwanzo wa daraja la ushirikiano, kuboresha ubadilishanaji mawazo na ujuzi kati ya kamati ya mipango ya bunge ya Zambia na ujumbe nilioandamana nao kutoka Kenya.” alisema Wetangula.

Mheshimiwa Wetangula alikuwa ameandamana na kiranja wa wengi katika bunge la taifa Sylvanus Osoro na naibu karani wa bunge la taifa Bw. Jeremiah Ndombi.