Home Habari Kuu Wetang’ula akutana wanaotishiwa kufurushwa shambani Kitale

Wetang’ula akutana wanaotishiwa kufurushwa shambani Kitale

0

Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula amefanya mazungumzo siku ya Jumamosi na waakilishi wa watu wanaotishiwa kufurushwa katika kipande kimoja cha ardhi mjini Kitale kaunti ya Tranz nzoia .

Watu hao wamepewa agizo la kuhama katika shamba la idara ya magereza mjini Kitale.

Wetang’ula amesena amepokea rasmi malalamishi ya kundi hilo linalotokana kusitishwa kwa agizo la kuhamishwa katika ardhi hiyo ambayo wamekuwa wakiishi kwa zaidi ya miaka 50.

Spika aliahidi kutafuta suluhu ya kudumu kwa mzozo huo na kuwashukuru kwa ushirikiano na uvumilivu katika swala hilo tete.

Wetang’ula aliandamana na seneta wa Trans Nzoia Senator Allan Chesang, wabunge Hon Ferdinand Wanyonyi wa Kwanza na Robert Pukose wa Endebes,waziri wa zamani Noah Wekesa na aliyekuwa Seneta Henry Ole Ndiema.

Website | + posts