West Ham United wamekatalia mbali ofa ya pauni milioni 90 kutoka kwa Arsenal kama ada ya kumsajili mwanandinga Declan Rice.
Westham ambao ni mabingwa wa kombe la Europa Conference League, wamesemekana kuwa radhi kumwachilia Rice kugura kwa ofa kubwa wakisubiria dau kutoka kwa mabingwa wa Ulaya Manchester City na mabingwa wa Ujerumani,Bayern Munich.