Home EURO 2024 Wenyeji Ujerumani na Uhispania kumenyana kwa robo fainali

Wenyeji Ujerumani na Uhispania kumenyana kwa robo fainali

0
kra

Timu za Ujerumani na Uhispania zitachuana leo ijumaa katika robo fainali ya kipute cha bara Ulaya.

Mchuano huo wa saa moja usiku, unatarajiwa kuwa wa kufa kupona ingizingatiwa kuwa timu zote zina wachezaji nyota na wenye ufundi mkubwa.

kra

Pia, timu hizo hazina majeraha ya kutisha.

Mabingwa hao mara tatu kila mmoja walishiriki fainali ya mwaka 2008 huku Uhispania ikiibuka mshindi.

Robo fainali ya pili itakuwa saa nne usiku baina ya Ureno yake Christiano Ronaldo na mabingwa mara mbili Ufaransa yake Kylian Mbappé.

vile vile, mtanange huo utakuwa wenye msisimko kutokana na uweledi wa timu hizo na nyota wake.

Timu hizo zilichuana kwenye fainali ya 2016 nchini Ufaransa ambapo Ureno ilishinda.

Boniface Mutotsi
+ posts