Waziri wa ardhi Alice Wahome amewapiga kalamu maafisa wa wawili katika wizara ya ardhi wa kaunti ya Nairobi, kwa madai ya kuwasaidia waekezaji wa kibinafsi kunyakua shamba la umma.
Wahome samesema mmoja wa maafisa hao alimsaidia mwekezaji wa kibinafsi kunyakua ardhi ya umma, huku wa pili akitoa ushahidi wa uongo mahakamani uliomsaidia mwekezaji wa kibinafsi anyakue ardhi ya umma.
Waziri ametoa tahadhari kwa wanyakuzi wa ardhi na wafanyikazi wa umma watakaowasaidia wanyakuzi wa ardhi kutwaa ardhi ya umma, akisema watachukuliwa hatua kali za kisheri.
Waziri Wahome alisema haya mapema Jumamosi alipotwaa ardhi ya makaburi iliyokuwa imenyakuliwa na mwekezaji wa bininafsi mjini Thika.
Waziri aliandamana na mbunge wa Thika Alice Ng’ang’a na katibu wake Nixon Korir.