Home Taifa Waziri wa Leba akutana na viongozi wa walimu kujaribu kuepusha mgomo

Waziri wa Leba akutana na viongozi wa walimu kujaribu kuepusha mgomo

0
kra

Waziri wa Leba Dkt. Alfred Mutua leo amefanya mkutano leo na viongozi wa chama cha walimu nchini, KNUT katika hatua iliyonuiwa kuepusha mgomo wa walimu.

Katika taarifa, Mutua alifichua kwamba alikutana na viongozi kadhaa wa chama cha KNUT akiwemo katibu mkuu Collins Oyuu na Patrick Munuhe ambaye ni mwenyekiti wa kitaifa.

kra

Walimu walikuwa wametishia kugoma kufuatia malalamishi kadhaa kama vile nyongeza ya mishahara kwa kiwango cha kati ya asilimia 7 na 9 kulingana na makubaliano ya pamoja ya mwaka 2021.

Wanalalamikia pia hatua ya serikali ya kuchelewa kutekeleza yaliyomo kwenye makubaliano hayo kama bima ya afya, kutowasilishwa kwa makato yao kwa vyama vya ushirika na kucheleweshwa kwa malipo ya kustaafu ya walimu.

Waziri Mutua hakusema iwapo waliafikia makubaliano ya kusitisha mgomo unaonukia.

Vyama vya walimu KNUT na KUPPET vilitoa ilani ya siku saba ya mgomo iwapo serikali haitatekeleza matakwa yao kufikia wakati wa kufunguliwa kwa shule.

Suala la kuajiriwa kwa walimu wa Junior Secondary kwa masharti ya kudumu pia ni mojawapo ya malalamishi ya walimu hao.

Website | + posts