Home Taifa Waziri wa Fedha akabidhiwa mswada wa mafao ya kustaafu ya majaji

Waziri wa Fedha akabidhiwa mswada wa mafao ya kustaafu ya majaji

0

Idara ya mahakama imewakabidhi maafisa wa Wizara ya Fedha wakiongozwa na Waziri Prof. Njuguna Ndung’u Mswada wa Mafao ya Kustaafu ya Majaji, 2024. 

Mpango huo uliopendekezwa unajumuisha marupurupu yaliyobainishwa, posho ya nyumba katika mishahara ya uzeeni, kima cha chini cha pensheni kwa mahakimu wasio na uwezo, bima ya matibabu, ruzuku ya gari baada ya kustaafu na angalau afisa mmoja wa usalama.

Kwa zaidi ya miaka 30, juhudi za kuanzisha mpango tofauti wa pensheni kwa majaji zimeonekana kupata vikwazo kama vile ukosefu wa kuungwa mkono na sheria.

Wakati watumishi wengine wa umma wamehamia Mpango wa Malipo ya Uzeeni wa Utumishi wa Umma, majaji na walimu wamesalia chini ya Sheria ya Pensheni ya mwaka 1946.

Mswada huo mpya unalenga kuzifanya nafasi za kimahakama zivutie kwa kutoa pensheni zinazoonyesha hali ya kipekee ya kazi zao.

Kwa sasa, umri wa majaji kustaafu ni miaka 70.

Kulingana na utafiti wa jopokazi uliofanywa katika nchi za Jumuiya ya Madola, hitaji la sheria maalum ya pensheni kwa majaji iliangaziwa huduma zao za kipekee kusisitizwa.

Rahab Moraa
+ posts