Home Kimataifa Waziri Owalo kugharimia masomo ya mwanafunzi wa Maseno School

Waziri Owalo kugharimia masomo ya mwanafunzi wa Maseno School

0
kra

Waziri wa Mawasiliano na Uchumi Dijitali Eliud Owalo kupitia kwa wakfu wake amejitolea kugharimia masomo ya mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya upili ya Maseno.

David Odhiambo Muga alipata alama 399 katika mtihani wa kitaifa wa darasa la nane, KCPE na kujipatia nafasi katika shule hiyo ya Maseno lakini wazazi wake hawakuwa na uwezo wa kumlipia karo.

kra

Muga alichukua hatua ya kuomba usaidizi kupitia mitandao ya kijamii, ombi ambalo lilimfikia waziri Owalo ambaye sasa ameamua kumsaidia.

Leo asubuhi, Owalo alitoa hundi ya shilingi elfu 98,654 kwa mwalimu mkuu wa shule ya Maseno Peter Owino, pesa ambazo ni karo ya kidato cha kwanza.

Pesa hizo zinajumuisha gharama za karo, ada ya maendeleo, usaidizi wa wazazi, sare za shule, godoro na mahitaji mengine.

Wakfu wa Eliud Owalo ulitoa mchango wa shilingi elfu 50 kwa mama mzazi wa Muga ili aanzishe biashara ya kuwezesha familia yake kujikimu kimaisha.

Alipokwenda kuwasilisha pesa hizo katika shule ya Maseno, Owalo alikuwa ameandamana na wanafunzi wa zamani wa shule hiyo Emmanuel Ombaka, Dennis Osano Kute na Barack Kamire.

Muga naye alisindikizwa na wazazi wake mama Ruth Addah Agola na babake Joseph Muga Owera, chifu wa nyumbani kwao Fred Omino na naibu chifu Agnes Otieno.

Mkurugenzi wa elimu katika eneo hilo Nelson Sifuna, mkurugenzi wa elimu katika kaunti Rosemary Birenge, mwenyekiti wa bodi ya usimamizi ya shule hiyo Daktari Olango Onudi na naibu Kamishna wa Kisumu Magharibi Bwana Wanyonyi pia walikuwepo.

Website | + posts