Waziri Owalo azindua mtandao wa WiFi katika soko la Magunga

Marion Bosire
1 Min Read

Waziri wa Habari na Mawasiliano Eliud Owalo jana Jumapili alizindua mtandao wa WiFi katika soko la Magunga eneo bunge la Suba Kusini katika kaunti ya Homabay. 

Kituo hicho cha mtandao wa bure wa umma ni mojawapo ya mitandao elfu 25 ambayo serikali inapanga kuzindua kote nchini kupitia kwa Wizara ya Habari na Mawasiliano.

Hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa ajenda ya serikali ya Kenya Kwanza ya kuhakikisha uwepo wa mfumo digitali kuambatana na mpango wa mabadiliko ya kiuchumi ya kutokea chini kuelekea juu almaarufu “Bottom-Up Economic Transformation Agenda – BETA”.

Dhamira ya kuzindua WiFi ni kuwezesha wamiliki wa biashara ndogo katika soko hilo kujihusisha na biashara mtandaoni wakati huu ambapo uchumi dijitali unaibukia nchini Kenya.

Waziri Owalo alikuwa ameandamana na spika wa bunge la taifa Moses Wetang’ula, naibu kamishna wa kaunti katika eneo la Suba Sebastian Okiring’, Gavana wa zamani wa Nairobi Evans Kidero, mbunge wa eneo la Suba kusini Caroli Omondi, John Odek ambaye ni mwanachama wa bodi ya chuo cha Utalii, mwenyekiti wa baraza la wazee la Kaksingri Nelson Ounga, Ken Obuya na Ben Onyango kati ya wengine.

Website |  + posts
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *