Waziri Owalo atoa msaada wa sare kwa Kenya Morans

0

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali Eliud Owalo, alitoa msaada ya sare za kuchezea kwa timu ya taifa ya mpira wa kikapu ya wanaume maarufu kama Kenya Morans.

Waziri Owalo aliitembelea timu hiyo Jumatano jioni katika uwanja wa taifa wa Nyayo ambapo inafanyia mazoezi.

Morans wanajiandaa kwa mechi za kufuzu kwa mashindano ya FIBA Afrobasket ya mwaka ujao, mechi hizo zikitarajiwa kuchezwa kuanzia baadaye mwezi huu.

Owalo alitoa changamoto kwa Morans kufuzu kwa mashindano ya mwaka ujao huku akiahidi kuendelea kuinga mkono kwa hali na mali.

Waziri aliandamana na mwenyekiti wa shirikisho la mpira wa kikapu nchini, KBF Paul Otula kocha mkuu wa Morans.