Home Kaunti Waziri Owalo atoa kambi ya matibabu Rarieda

Waziri Owalo atoa kambi ya matibabu Rarieda

0

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali Eliud Owalo ametoa kambi ya bure ya matibabu kwa wakazi wa Rarieda.

Kambi hiyo ya kwanza inafadhiliwa na wakfu wa Eliud Owalo na itaandaliwa Disemba 23, katika Lwak na kituo cha kimisheni cha Lwak.

Kwa mujibu wa Waziri Owalo, kambi hiyo itasaidia kukabiliana na magonjwa madogo madogo ambayo huwatatiza wenyeji wa Rarieda kama vile shinikizo la damu, kisukari, magonjwa ya moyo, saratani, kupimwa magonjwa ya figo na afya ya uzazi.