Home Kimataifa Waziri Owalo amwomboleza mwanahabari Mutegi Njau

Waziri Owalo amwomboleza mwanahabari Mutegi Njau

0
kra

Waziri wa mawasiliano na uchumi dijitali Eliud Owalo, amemwomboleza mwanahabari mkongwe Mutegi Njau ambapo amesema alipokea habari za kifo chake kwa huzuni kubwa.

“Mutegi ambaye alifanya kazi kama mwanahabari kwa miongo minne kwenye kampuni za Royal Media Services, Nation Media Group na KBC, alikuwa mwanahabari aliyejitolea, mtetezi shupavu wa ukweli na wa uhuru wa vyombo vya habari.” aliandika Owalo kwenye taarifa.

kra

Owalo alielezea kwamba ana kumbukumbu za wakati alikutana na Njau hasa kwenye mahojiano katika runinga ya Citizen inayomilikiwa na Royal Media Services.

Alikiri kwamba ushawishi wake utamotisha vizazi vijavyo vya wanahabari huku akitoa pole zake kwa familia yake, marafiki na wanahabari wote nchini.

Familia ya Mutegi Njau ilitangaza kwamba alikata roho usiku wa Alhamisi Juni 27, 2024 kunako saa moja jioni.

Aliwahi kufanya kazi na shirika la utangazaji nchini KBC kabla ya kuhamia shirika la habari la Nation ambako alihudumu kwa muda wa miaka 24 kisha akaondoka mwaka 2005 a kujiunga na Royal Media Services alikohudumu hadi alipostaafu.