Home Michezo Waziri Owalo ajaribu kusuluhisha zogo la Gor Mahia na FKF

Waziri Owalo ajaribu kusuluhisha zogo la Gor Mahia na FKF

0

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali Eliud Owalo ameandaa mkutano na maafisa wa klabu ya soka ya Gor Mahia na wale wa shirikisho la kandanda nchini, FKF.

Kupitia mitandao ya kijamii, Owalo alisema aliamua kuchukua hatua hiyo kama shabiki sugu wa Gor Mahia ili kujaribu kusuluhisha zogo lililopo.

Waliowakilisha Gor Mahia kwenye mkutano wa leo ni mwenyekiti Ambrose Rachier, naibu wake Francis Wasuna, katibu Sam Ochola na mwanachama wa kamati maalumu Gerphas Okuku.

FKF nayo ilikawakilishwa na mkurugenzi mkuu Barry Otieno, mkuu wa kitengo cha mashindano na utoaji leseni Doreen Nabwire pamoja na Grace Shauri.

Tatizo lilianza pale FKF ilipoamua kufutilia mbali leseni ya klabu ya Gor Mahia kutokana na madai ya kukosa kulipa wachezaji marupurupu yao.

Gor, hata hivyo, inashikilia kwamba kufikia sasa imelipa pesa ilizokuwa inadaiwa na wachezaji na kutoa ushahidi wa hati za malipo lakini FKF haijabadili msimamo.

Kulingana na Owalo, majadiliano ya mara kwa mara na wadau ni muhimu katika kuendesha fani yoyote ile ya michezo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here