Home Michezo Waziri Owalo aituza Gor Mahia shilingi milioni 2 kwa kushinda ligi

Waziri Owalo aituza Gor Mahia shilingi milioni 2 kwa kushinda ligi

0
kra

Waziri wa Habari na Mawasiliano Eliud Owalo amewatuza mabingwa wa ligi kuu Gor Mahia shilingi milioni 2 huku akiwapa changamoto ya kusajili matokeo bora barani Afrika.

Owalo alisema haya Jumatatu alipoandaa dhifa ya chakula cha mchana kwa timu hiyo baada ya kunyakua taji la 21 la ligi kuu siku ya Jumapili.

kra

Waziri pia aliwashauri wachezaji wa timu hiyo kusalia kikosini kwa muda mrefu ili kuafikia matokeo bora.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na maafisa wakuu wa timu hiyo akiwemo aliyekuwa kocha Jonathan McKingstry na mweyekiti Ambrose Rachier miongoni mwa wengine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here