Home Habari Kuu Waziri Nakhumicha: Malipo ya NHIF yatapungua hadi shilingi 300

Waziri Nakhumicha: Malipo ya NHIF yatapungua hadi shilingi 300

0
Waziri wa afya Susan Nakhumicha.

Waziri wa Afya Susan Nakhumicha amesema ada za bima ya matibabu, NHIF zitapungua hadi shilingi 300 kuanzia mwezi Septemba mwaka huu.

Kulingana naye, hii ni sehemu ya marekebisho yanayotekelezwa katika sekta ya afya.

Waziri ambaye alikuwa akizungumza katika kaunti ya Bungoma, alisema mgao wa sekta ya afya katika bajeti ya mwaka huu utawezesha utekelezaji wa marekebisho kadhaa kama vile huduma kwa kina mama wajawazito.

Alisema mpango wa Linda Mama umetengewa shilingi bilioni 4.1 mwaka huu wa kifedha.

Nakhumicha alisema serikali ya Kenya Kwanza inaendeleza marekebisho katika shirika la kusambaza bidhaa za matibabu, KEMSA na usimamizi wa NHIF huku ikiwekeza katika kuwezesha wahudumu wa afya.

Nakhumicha alikiri kwamba mambo mengi yalikwenda kombo katika Wizara ya Afya hata kabla ya kuteuliwa kwake kuiongoza lakini sasa mipango inatekelezwa ya kuyarekebisha.

Alisema wamefanikiwa kulainisha KEMSA na sasa wanaangazia NHIF ambapo hivi karibuni watateua mkurugenzi mtendaji mpya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here