Home Habari Kuu Waziri Nakhumicha aongoza maadhimisho ya TB nchini

Waziri Nakhumicha aongoza maadhimisho ya TB nchini

0

Waziri wa afya Susan Nakhumicha amesema kuwa mpango wa afya mashinani wa mwaka wa 2023 -2030 dhidi ya ugonjwa wa TB kwa ushirikiano na washika dau, una manufaa makubwa kwa vita dhidi ya ugonjwa huo.

Akizungumza Katika hafla ya kuadhimisha siku ya TB duniani katika kaunti ya Muranga, Nakhumicha alisema mpango huo utawezesha wagonjwa wa TB kujulikana mapema na kutibiwa.

Waziri alieleza kuwa asilimia 27 ya wagonjwa wa TB wanasumbuka kutokana na gharama za matibabu ya ugonjwa huo na hivyo serikali itafanya juhudi kujumuisha tiba ya TB katika fedha za mpango wa afya kwa wote.

Aliongeza kwamba serikali inatia bidii ili kenya iwe nchi huru kutokana na TB. Hivyo inahakikisha huduma zake ni nafuu na zinapatikana kwa wakenya wote bila kujali wanapoenda kupata huduma za afya’’.

Alifichua kwamba serikali imetuma wahudumu elfu 107 wa afya ya jamii kote nchini kama mojawapo ya hatua za kudhibiti ugonjwa huo ambao ni wa nne kwa kusababisha maafa nchini.

Amewataka wananchi kujiandikisha kupimwa ili kutibiwa mapema iwapo watapatikana nao.

Hafla hii pia ilihudhuriwa na Gavana wa Muranga Irungu Kang’ata.

Kauli ya maadhimisho ya mwaka huu ni Ndio! Twaweza maliza TB!

Boniface Mutotsi
+ posts