Waziri wa Biashara,uwekezaji na viwanda Salim Mvurya, amefungua rasmi maonesho ya kibiashara ya Indonesia jijini Nairobi maarufu kama Indonesia Nairobi Expo (INDONEX) 2024,kuadhimisha miaka 45 ya ushirikiano wa kibiashara na Kidiplomasia kati ya Kenya na Indonesia .
Indonesia ni mshirika wa kibiashara wa Kenya katika uagizaji bidhaa kama vile mashine ,nguo na mafuta ya mawese.
kwa upande wake Kenya huuzia Indonesia bidhaa kama vile chai,kahawa na bidhaa za kilimo cha bustani.
Waziri amesisitiza haja ya kuimarisha ushirikiano zaidi katika nyanja ambazo zimesahaulika kama vile usindakaji wa bidhaa za kilimo,nguo,dawa,na viwanda vya kuongeza thamaniambavyo ni muhimu kwa ukuzaji uchumio na kubuni nafasi za ajiri nchini Kenya.