Home Habari Kuu Waziri Mutua akosoa wanaopinga Mswada wa Fedha 2024

Waziri Mutua akosoa wanaopinga Mswada wa Fedha 2024

0
kra

Dkt. Alfred Mutua ambaye ni Waziri wa Utalii na Wanyamapori nchini ameonyesha kutoridhika kwake na wanaopinga Mswada wa Fedha wa mwaka 2024.

Dkt. Mutua alitaja matendo yao kuwa yaliyotekelezwa bila yao kuwa na ufahamu kamili wa mambo muhimu.

kra

Akizungumza huko Narok wakati wa kuzindua mpango wa mwaka huu wa sensa ya wanyamapori, Dkt. Mutua alisisitiza kwamba mswada huo ulipitia mchakato stahiki bungeni na vipengele vyote tata vikarekebishwa kufuatia maoni ya wananchi.

“Maandamano hayafai kwa sababu matakwa ya waandamanaji tayari yameshughulikiwa,” alisema Waziri huyo akiongeza kuwa Wakenya wanafaa kukubali changamoto za kiuchumi za taifa hili ambazo zinalazimu kufanywa kwa maamuzi magumu.

Huku akikiri kwamba matozo ya ushuru yaliyopendekezwa sio ya kawaida, Mutua alisema matozo hayo ni lazima yatekelezwe ili kufadhili mipango ya serikali.

Aliwataka Wakenya kuwa na subira wakati serikali inajizatiti kuimarisha uchumi.

Vile vile alionyesha wasiwasi kuhusu kile alichokitaja kuwa tabia inayozidi kuonekana ya Wakenya kutoheshimu maafisa wa usalama akigusia kisa cha afsa wa polisi kupoteza mikono yake kwenye maandamano ya jana jijini Nairobi.

Waziri huyo pamoja na Gavana wa Narok Patrick ole Ntutu wameahidi kutoa mchango wa shilingi milioni moja kwa familia ya afisa huyo aliyeumia kugharimia matibabu.

Mutua alionya dhidi ya maandamano yanayoendeshwa na uanaharakati na mambo yasiyo ya kweli.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here