Home Biashara Waziri Miano: Sekta binafsi ni muhimu kwa ukuaji uchumi Afrika

Waziri Miano: Sekta binafsi ni muhimu kwa ukuaji uchumi Afrika

0

Waziri wa Jumuiya ya Afrika wa Kenya Rebecca Miano amesisitiza umuhimu wa sekta binafsi katika kuhamasisha ukuaji wa uchumi kitaifa, kikanda na katika ngazi za bara la Afrika. 

Miano amesema sekta ya kibinafsi inachangia asilimia 80 ya jumla ya uzalishaji barani Afrika, theluthi mbili ya uwekezaji na robo tatu ya mikopo mbali na kuajiri asilimia 90 ya watu wanaofanya kazi barani humo.

Waziri alisema sekta binafsi ambayo ni imara ni muhimu katika kufikia mabadiliko endelevu ya kiuchumi barani Afrika.

“Mafanikio ya ukuaji uchumi wa Afrika yamejikita kwa wajibu wa sekta binafasi katika kufikia malengo ya ukuaji wa chumi za Afrika, na pia kubuni mali nyingi na kuongeza nafasi za ajira,” alisema Miano.

Alitoa wito kwa Jumuiya za Kiuchumi za Kikanda za Afrika, ikiwemo EAC, kuongeza uwekezaji katika viwanda vya kilimo na uziduaji kupitia uongezaji thamani ili kupanua uwezo wa mitungo yote ya uongezaji thamani.

“Mitungo ya uongezaji thamani ni muhimu kwa kuhamasisha biashara baina ya nchi za Afrika, ukuaji wa pamoja wa kiuchumi na maendeleo ya kiviwanda,” alisema Miano.

Waziri aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 14 la Sekta Binafsi la Kiwango cha Juu la Umoja wa Afrika katika Jumba la Mikutano ya Kimataifa la KICC, Nairobi.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here